LADY JAY DEE NA CLOUDS

Hivi karibuni kumezuka mgogoro mkubwa baina ya msanii Lady jay dee na kituo cha redio cha clouds fm kutokana na kituo hicho kutopiga nyimbo yake mpya ya jotohasira.Hizi ni baadhi ya tweets za lady jay dee akikishutumu kituo hicho na baadhi ya wasanii
 ''Radio ya watu isyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu,wasiopendwa na watu''.

''Wasanii wa THT walikatazwa kuja kuimba nyumbani lounge na boss wao mbali na kuwa walishalipwa hela za advance.Linah na Ben Paul mnabishwa hamkukatazwa?Nisalitini ila hamtopata faida mtatoka kapa pia''
''Walidhani ni show yangu wakafikiri nitatajirika,ila nilitoa ukumbi tu wakamsaliti aliyeandaa show.Not me"
Anaendelea:
 '' Kill me if you can,am on fire siogopi ng'oo jipangeni.Ni kweli nimelamba sumu lakini hainidhulu,nakunywa maziwa daily I will survive''
''Hee! kuna wajinga wanadhani nili tweet nikiwa nimelewa,nilimaanisha na msimamo ni  huo huo,sitasema oh kuna mtu ka hack account yangu,nooo its me".
 ''Mungu sio Ruge wala Kusaga" No surrender.Confidence"

Maoni yangu kama blogger:
Up to here i respected jay dee so much ila swali ni ''Je,alikuwa wapi muda wote kuyasema haya?''alipokuja kunikata maini ni pale kuwa kipindi cha nyuma alikuwa na mengi ya kuzungumzia lakini uhalisia ulikuwa unambana,alikuwa hayuko mbali kimaisha hivyo alikuwa hawezi kufungua  mdomo wake ila kwa kuwa sasa anajiweza hakuna haja ya yeye kuendelea kunyanyasika.
Hapa ndipo tunapofeli watu wengi umimi,ubinafsi na kujiangalia mwenyewe ndo kunakoturudisha nyuma.Lady jay dee yuko clouds siku nyingi na kama ni hayo matatizo basi aliyaona siku nyiingi iweje aanze kulalamika leo?.Ulikuwa unanyamaza ukingoja kituo hicho hicho unachokiita chenye unyanyasaji kikulee,kikutoe ndipo ukigeuke na kuuelezea huo uovu unaosema umeuona siku nyingi?.Kama uovu/unyanyasaji huo upo siku nyingi kama unavyodai ina maana hata wewe umetoka kupitia unyanyasaji huo.Kwamba inabidi ukubali kuwa kupitia kule wengine kunyanyasika na kubaniwa wakati kituo hicho kinakulea wewe ndiko kulikotengeneza njia ya wewe kufika mbali.Hivi inawezekana kweli kuiangusha nguzo iliyokulea miaka yote?Ni sawa na leo mtu uutafute uongozi kupitia chama fulani na unaona kabisa chama hicho kinatumia rushwa kuupata uongozi na unaamua kuendelea nacho kwasababu unautaka uongozi kwa mpango kwamba kitakapokuwezesha kufika utakapo basi utaanza kupambana na hiyo rushwa iiyokufikisha hapo.Inawezekanaje?.Ukitaka kuangamiza kitu basi uanzie kwenye mizizi sio eti unyamaze kimya usubiri baadae ukifika kwenye matawi unakotaka ndo uanze mapambano .Jamani nyie watu kama ulilelewa na rushwa utabaki kuwa wa rushwa tu.Kama ulikuzwa na unyonyaji  na wewe utabaki kuwa mnyonyaji wa wengine pia.Huo ndio u binafsi wenyewe na kwa style hii hatuwezi kufika mbali hadi tubadilike.Mtu huwezi kuwa umepata maendeleo kupita rushwa/unyonyaji fulani ulioukalia kimya siku zote kwa maslahi yako binafsi afu baadae uanze kuvipiga vita wakati damu na maendeleo yako yote yana harufu ya hiyo rushwa/uanyonyaji wenyewe.Halafu unawezaje kuwalaumu wengine kama akina Linah because they are not supporting you?Wewe uliuona unyanyasaji ukaunyamazia kimya kwasababu ulitaka utoke kwanza, don't you think they are using the same technique you used years back before you were able to stand on your own?I am not supporting anybody but mimi nadhani hawa akina Linah unaowazungumzia kosa lao ni kufuata nyayo/mfano wako uliouonyesha wewe uliowatanguliaJamani mtu huipendi rushwa ikemee from the get go without caring umefika ulikotaka ama la.Huupendi unyanyasaji upigie kelele tangu unapoanza kuuona sio uukumbatie afu ukulee afu baadae ndo uanze kupigana nao...
Let only the clean ones point the dirty ones....!
  

No comments:

Post a Comment