Direct from Bungeni hours ago:MBUNGE GODBLESLEMA APEWA SIKU 7 KUJIELEZA

Mbunge wa Arusha mjini, Mh. Godbless Lema apewa siku 7 na Naibu spika kumtaka  kutengua kauli yake aliyoitoa masaa machache yaliyopita bungeni akimuelezea Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama muasisi na kinara wa migogoro ya kidini inayoendelea hapa nchini.Alipotakiwa kuthibitisha hilo Mh. Godbless Lema aliuelezea udhaifu wa Mh. Jakaya Mrisho wa kushindwa kutatua (according to yeye)mgogoro wa Geita baina ya wakristo na waislamu kuhusiana na nani achinje nyama.Nina-i report hii kama ilivyojiri bungeni.

 Maoni yangu :Mimi naona hapa Mheshimiwa mbunge amekosea sana kumtaja Rais kama kinara wa udini Tanzania kwa kutolea mfano ishu ya Geita.Siku chache zilizopita kuliibuka mgogoro mkubwa baina ya wakristo na waislamu kuhusiana na nani achinje nyama huko Geita.Viongozi mbalimbali wakiwemo Mh.Pinda na Mh.Wassira walitembelea(wakimwakilisha Mh.Jakaya Mrisho) kujaribu kutafuta ufumbuzi wa swala hili ili kuhakikisha mgogoro huu unakwisha na amani inakuwepo nchini.Hata hivyo uamuzi uliofikiwa na viongozi wetu ni kuwa;kutokana na nature ya mgogoro wenyewe kuwa wa kidini Mh. Pinda naWassira walikaa na viongoz wa kidini kuwaomba wakutane ili kupata suluhu ya mgogoro huo na kisha wapeleke ripoti itumike kama ushauri na mwongozo wa serikali jinsi ya kutatua tatizo hili, wakati suluhu inaendelea kutafutwa walishauri waislamu waendelee kuchinja nyama kama ilivyokuwa siku zote.Mh. Godbless Lema huu ndio unaouita ukinara wa udini wa Rais Jakaya Kiwete kweli??Kwa maoni yangu uamuzi uliotolewa ndio uliokuwa wa busara zaidi.Kama ni nyama wakristo tumekuwa tukila nyama zinazochinjwa na waislamu siku zote,kwanini leo ghafla tusile kama sio huo ndo uchochezi wa migogoro ya kidini wenyewe?Maamuzi ya muda yaliyofikiwa yalikuwa ni sawa kutokana na nature iliyopo kwamba mkristo anaweza kula nyama ilochinjwa na mwislamu ila mwislamu hawezi kula iliyochinjwa na mkristo sasa kuna ubaya gani kwa serikali kutoa tamko kwamba utamaduni huo uendelee hadi ufumbuzi ukipatikana?Huo ndo Mheshimiwa mbunge aliouita ni udini kwa kuanglia haraka haraka kuwa Rais ni muislamu basi tamko lililotolewa ni la kuu pendelea upanda mmoja.Je,alipaswa aseme waislamu wachinje ya kwao a wkristo wachinje ya kwao,msomaji unadhani nini kingetokea kama si kuligawa taifa kutokana na dini?Uamuzi uliotolewa kwa muda ni sahihi kabisa na umezingatia utamaduni ulio dominate siku zote mpaka leo kuwa waislamu ndio wachinjaji and christians had never had a problem before kula vilvyochinjwa na waislamu.Haikuhusiana na dhana yoyote ya Rais kuwa mwislamu na kuupendelea upande mmoja hivyo kuthibitisha kauli kuwa Mh. Jakaya Kikwete ni muasisi wa udini kutokana na uamuzi wa muda uliofikiwa kuhusu mgogoro wa Geita.Hadi sasaMh.Godbless Lema ametawa kufuta kauli yake ama kupewa siku 7 kupeleka ushahidi Bungeni kuhusu kauli  hiyo....

8 comments:

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  2. "Eti nina mpango wa kugombea ubunge baadae ndo mana nimefungua hii blog kwasbbu nataka kuitumia ku gain popularity ili nikiingia kwenye siasa isinipe shida'.Watu wanaangalia jina au wanaangalia sera?Ukampigia na 'Fredy' simu kumtaka akutafutie na kadi ya ccm..unamsumbua mtu usiku hujui kadi zinapopatikana.Ndo ukaona uhame na chama kabisa wakati juzi tu ulikuwa chdma au ndo tuseme skendo la lwakatare limekukimbiza chdma.RUDISHA kadi ya chdma kwanza kabla hujaomba ccm.Afu ubunge kwa siasa gani jamani hiyo uliyoijulia juzi jamii forum ama?

    ReplyDelete
  3. Dah Tanzania tutafika kweli kwenye maendeleo yenyewe! Blogger kaongea point kishenz,haijalishi mtu ni chadema au ccm,angelieni hoja jamani,yani watu moja kwa moja mmekimbilia kwenye vyama,Thats the first, and the 2nd,nyie moja kwa moja mnaonyesha michuki yenu kwa logger kwa sababu mnamjua personally, yani inaonyesha dhahir mlivyokua na upeo mfupi kama maisha ya funza, kwani hapo kuna uchadema na u ccm jamani, mtu kaongea mawazo yake, we kama huna mawazo kaa kimya tu, sio lazma muongee,maBOYA kweli nyie wote mliocomment hapo juu, yani waPUMBAVU kabisa.SHENZI

    ReplyDelete
    Replies
    1. a.k.a anonymous21 April 2013 at 10:21

      Tatizo watu wengine wana comment wakiwa wametoka kuvuta bangi tayari.Afu acheni kuvuta hizo bangi zenu afu mnakuja kutupia vipisi kona hii.Ona sasa mnatuunguzia blog yote inawaka moto.Ngoja nikachuke fire extinguisher nije kuzima huo moto then nitarudi baadae kuweka comment yangu kuhusu hiyo post

      Delete
  4. Kwani mtu akiwa chadema ndo manake hata chadema wakienda hovyo anatakiwa a support.Swala la uchama ndo linalolifikisha taifa pabaya siku zote.Mtu uko CUF mfano basi ndo hata wakifanya fujo zisizoeleweka unawasapoti tu mradi ni chama chako,unakumbatia ujinga.Lazma kuwa na kukosoana within chama husika chenyew ndo nchi itasonga mbele.Mtu unaangalia maslahi ya taifa bwana swala la chama changu pembeni

    ReplyDelete
  5. huo mtazamo umeutoa kama mwananchi au political analyst? kama umeutoa kama mwananchi wa kawaida ni sawa.....siwezi kukushangaa maana yawezekana baada ya maisha ya mtaani kukupiga umeanza kufuatilia siasa,umeanza sasa kufuatilia siasa ila rudi nyuma miaka minane iliyopita wakati kikwete anagombea urais alipoanzisha makundi na kuwabomoa wapinzani wake kisiasa.......udini,ukanda na ukabila ulitumika sana kuwapoteza kisiasa wagombea wengine......ila kama mtazamo wako ni kama political analyst,jua basi una uwezo mdogo sana kwenye kuijadili siasa ya tanzania......embu jiulize kwa nini hii migogoro imejitokeza wakati kikwete rais? leo hii inafikia hatua rais analalamika waislamu wamemsomea dua za kutaka kumuua hapo ujue kuna tatizo na chanzo cha huu mgogoro ni siasa zake za udini kutaka kuupata urais bila kufikiria mbele matatizo yatakayo kuja kuikumba nchi......ndio haya yanayotokea sasa...........

    ReplyDelete
  6. Chadema originale21 April 2013 at 11:36

    Ni wazi kabisa umeingia kwenye siasa juzi kama sio leo.Mdau hapo juu kula tano, unanidai mzinga wa jack daniels na castle lit mbili,sawa?Blogger kama ni kweli umeijulia siasa kupitia jamii forum basi pitia post za nyuma zooote jukwaa la siasa ndio uje u re-post hapa.Sina hakika ila kama ni kweli unapanga kugombea ubunge miaka ijayo,anza kuweka post za kisiasa zaidi humu tukunoe taratiiibu kwa ajili ya hicho kinyang'anyiro cha mwaka 2020 sijui.

    ReplyDelete
  7. mhhhh, yani nimekutana na matusi basi hamu yote imeisha. anyways dear blogger, mawazo yako sio mabaya na ya wengine yanakubalika. i hope wote humu ni watu wazima haina haja ya kuambiwa what they should do. take what is right na wenye matatizo na wewe achana nao. big up gal. ntakutafuta weekend

    ReplyDelete