MNAOWANIA URAIS MSIKUBALI KUPOKEA PESA ZA HUYU MFANYABIASHARA FISADI AMBAYE PIA NI KINARA WA MADAWA YA KULEVYA



Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Reginald Mengi ametoa ya moyoni kwa wote wenye mpango wa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka miwili ijayo.


Bwana Mengi ameyatoa maombi yake ya moyoni na kuyaweka hadharani kupitia akaunti yake ya twitter, na hiki ndicho alichokiandika;



“Nawaombea Mungu wanaotaka Urais wasipokee mshiko wa mfanyabiashara fisadi mkubwa ambaye pia ni kinara wa madawa ya kulevya.”




Mfanyabiashara ambaye Mengi anamzungumzia hapo ni nani,ndo kwenye utata.Hilo linaweza kuwa ni jiwe gizani kama mlengwa yupo basi ujumbe utakuwa umemfikia ingawa mpaka sasa sielewi kwa hakumtaja kwa jina kabisa angali ana hakika na jambo hilo analolizungumzia.Unajua wanasema always truth,if you can prove it, is an absolute defense to a defamation claim

1 comment:

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete